Mwanamume mwenye watoto wanane amehukumiwa kifo baada ya kupatikana na kosa la mauaji.
Mshukiwa, Elisha Nelson Mwaruwa, anadaiwa kumuua kwa kumkata mara tatu shingoni mzee wa miaka 65 huko Samburu, mnamo Agosti 24, 2014.
Akitoa hukumu hiyo siku ya Jumatano, jaji Martin Muya alisema kuwa kutokana na ushahidi uliotolewa ni wazi kuwa mshukiwa huyo alihusika katika mauaji hayo.
Mshukiwa aliambia mahakama kuwa walikuwa na mzozo wa ardhi na mwendazake na alijipata amemuua mwendazake baada ya nyumba na mimea yake kuharibiwa na mzee huyo.
Aidha, mshukiwa alijisalimisha kwa polisi na kwa jamii baada ya kutekeleza mauaji hao.
Mshukiwa huyo ana siku 14 za kukata rufaa kupinga hukumu hiyo.