Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Mwanamume mwenye umri wa makamo amefikishwa mahakamani na kufunguliwa mashtaka ya kupatikana na kaseti zenye mawaidha ya itikatidi kali.

Upande wa mashtaka uliambia mahakama siku ya Jumatatu kuwa mnamo Februari 5, 2016, mshukiwa, Ibrahim Mafudh Ashur alipatikana na kanda moja yenye mafunzo ya marehemu Aboud Rogo, yanayodaiwa kuwa ya itikadi kali na kupigia debe kundi la kigaidi la al-Shabaab.

Ashur alikanusha mashtaka hayo mbele ya Hakimu Richard Odenyo.

Kesi yake itatajwa Machi 31, 2016, ili kuwasilishwa ombi la dhamana.