Share news tips with us here at Hivisasa

Mwanamume mmoja amefikishwa katika Mahakama ya Mombasa kwa madai ya kumnajisi mtoto wa miaka mitatu.

Mshukiwa, Yusuf Timene, anadaiwa kumbaka mtoto huyo mnamo Februari 7, 2016 katika eneo la Miritini.

Mtuhumiwa alikana madai hayo mbele ya Hakimu Daina Mochache siku ya Jumatano.

Hakimu Mochache aliamuru mshtakiwa kuwekwa kizimbani akisuburi kusikilizwa kwa kesi yake mnamo Machi 21, 2016.