Mwanamume mmoja alifikishwa katika mahakama ya Nyamira na kushtakiwa kwa madai ya kumnajisi mtoto wa umri wa miaka 9 katika kijiji cha Nyabisimba kaunti ya Nyamira.
Mshukiwa huyo kwa jina Edward Oteki alifikishwa mahakamani siku ya Jumanne mbele ya jaji wa mahakama hiyo Ruth Gitagwa na kushtakiwa kwa kosa la unajisi.
Wakati huo huo, iliripotiwa kuwa mshtakiwa huyo anadaiwa kutekeleza uovu huo mnamo Disemba 11, 2015 katika kijiji cha Nyabisimba.
Aidha, mshtakiwa huyo alikana kosa hilo mbele ya jaji wa mahakama hiyo na baadaye akaachiliwa kwa dhamana ya shillingi 150,000.
Kesi hiyo itasikizwa tena mnamo Januari 19, 2016.