Polisi eneo la Ndithini wanamzuilia mwanamume was miaka ishirini na mitatu kwa sababu ya kuwatishia mara kwa mara kuwaua wazazi wake.
Akidhibitisha kisa hiki, naibu was chifu was Kikole Philip Musyoka alisema kuwa kijana huyu amekuwa akiwatishia kuwaua wazazi wake kwa muda mrefu, jambo ambalo limepelekea wazazi hao kuishi na hofu ya hatma ya maisha yao.
Chifu huyo alielezea kuwa kijana huyu atachunguzwa ili kubaini iwapo ana akili timamu ili hatua inayofaa kuchukuliwa.
"Kijana huyo amekuwa akitishia kuwaua wazazi wake, jambo ambalo limekuwa likiwakosesha lepe la usinginzi huku wakihofia kushambuliwa, lakini sasa watapata amani kuanzia leo," alisema Musyoka.
Chifu Musyoka alielezea kuwa wazazi wa mwanamume huyo, walikuwa wakipuuzia matisho yake kwa muda mrefu bila kujua hatari iliyopo.
Mwanamume huyo anasubiria kufikishwa mahakamani hii leo, Jumatano.