Mwanamume wa umri wa miaka hamsini anaendelea kuuguza majeraha ya mgongo katika hospitalii ya Embu level four baada ya kukatwa kwa panga na mwanamke mmoja mwenye umri wa miaka 30 baada ya wawili hawa kugombana siku ya ijumaa.
Kwa mujibu wa chifu wa kata ya Kivaa Josphat Mutiso, mwanamume huyu alikuwa amekubali agizo la kumlimia mwanamke huyo shamba lake, lakini akaghairi na kukosa kuenda kinyume na maelewano yao.
Mwanamume huyo alivamiwa kwa upanga baada ya kufika nyumbani kwa mwanamke huyo ili kueleza kilichomfanya asitimize ahadi kama walivyosikizana.
"Baada ya kukosa kutimiza ahadi kama walivyoelewana mwanamume huyo alienda kwa mwanamke huyo kujieleza lakini wakakosa kusikizana pale mwanamke hugo alimvamia na kumkata mgongo kwa upanga," alisema Wambua.
Majirani walioskia ukemi walimkimbiza mwanamume huyo katika hospitali ya Kivaa health centre alipopewa huduma ya kwanza kabla ya kuhamishwa katika hospitali ya Embu.
Vilevile chifu huyo aliwaomba wakaazi kutozua vurugu na kuumizana wanapogombana bali kujifunza kutatua mambo kwa utulivu.
Mshukiwa huyo alitiwa mbaroni na maafisa was polisi na anazuiliwa katika kituo cha polisi cha Kaburu huku uchunguzi kuhusu kisa hicho ukiendelea ili kufikishwa mahakamani siku ya Jumatatu.