Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Mwanamume wa umri wa miaka hamsini alipata majeraha makubwa baada ya kuvamiwa na mamba katika mto wa Thika katika eneo la Uvouni kaunti ndogo ya Yatta. 

Akidhibitisha kisa hiki, chifu wa kata ya Kwa ndolo Peter Mutiso alisema kuwa mwanamume huyo alikuwa akioga katika mto huo mchana pale alivamiwa na mamba huyo na kumuuma mikono yote miwili. 

Aidha, chifu mutiso alisema kuwa mwanamume huyo aliokolewa na wakaazi waliomfukuza mamba huyo kwa mawe. 

Mwanamume huyo aliyepata majeraha makubwa alikimbizwa katika hospitali ya Matuu level four kupata matibabu. 

Chifu huyo aliwaonya wakaazi kuepuka kuogelea katika huo mto hasa wakati huu pale maji yamepungua kwani mamba hutokea na ni rahisi kuvamia watu. 

"Ingekuwa vyema watu waepuke kuogelea katika mto huo kwani mamba hukua kwa wingi na huweza kuvamia watu," alisema Mutiso.