Siku chache tu baada ya kutokea shambulizi kwa wanajeshi wa Kenya kule El Adde Somalia ambalo limepelekea vifo kadhaa vya majeshi ya Kenya, wito umetolewa kwa serikali kuondoa vikosi hivyo nchini humo.
Mwenyekiti wa ODM tawi la Nakuru Denis Okomol anasema kuwa wakati ni sasa wa taifa la Kenya kufikiria kuhusu kuondoa vikosi hivyo somalia.
"Hatuwezi endelea kupoteza wanajeshi wetu hivi. Nafikiri serikali inafaa kuwaondoa huko na walinde nchi yetu badala yake," alisema Okomol.
Mwenyekiti huyo wa ODM aidha anadai kuwa huenda kuna watu wanaonufaika wakati vikosi hivyo vinasalia Somalia.
"Huenda kuna wenye wananufaika kutokana na biashara haramu ya makaa na sukari, lakini wakati ni sasa kwa vikosi hivyo kuondoka Somalia," aliongeza Okomol.
Aliyasema haya siku ya Alhamisi wakati wa mahojiano mjini Nakuru.