Share news tips with us here at Hivisasa

Huku uchaguzi mkuu wa 2017 ukikaribia, mwenyekiti wa TNA Kaunti ya Nakuru Samuel Githaiga amewataka viongozi kuepuka siasa za ukabila.

Githaiga anasema kuwa iwapo viongozi hawatapima matamshi yao, basi huenda wakalitumbukiza taifa hili pabaya.

"Wito wangu kwa viongozi Nakuru ni kwamba wakati wa siasa za ukabila umepita, tunafaa kuyaunganisha makabila yote ya Nakuru," Githaiga alisema.

Wakati huo huo amesitiza kuwa chama cha TNA hakijavunjwa hadi pale kutakapokuwa na mwongozo kutoka kwa afisi kuu.

Kwa mujibu wake, afisi ya TNA ingali inashughulikia mikakati kadhaa kuhakikisha kwamba kutakuwa na uteuzi haki na huru chamani. Alikuwa akizungumza Alhamisi katika kikao na wanahabari mjini Nakuru.