Uhasama wa muda ambao umezidi kijidhihirisha kati ya pande mbili hasimu za kanisa la Evangelica Lutheran Church of Kenya (ELCK ) tawi la Nyamira unazidi kutokota.
Hii ni baada ya kundi moja hasimu kumuapisha rasmi askofu atakaye ongoza kanisa hilo tawi la Nyamira.
Kundi hilo hasimu linaloongozwa na Askofu Thomas Asiago na linalopinga uongozi wa aliyekuwa Askofu Mkuu wa kanisa hilo nchini Thomas Obare lilimwapisha Sospeter Okong'o huku likimlaumu Obare kwa mafarakano ya uongozi ambayo yamekuwa yakilikumba kanisa hilo kwa muda sasa.
"Tunamlaumu Askofu Walter Obare kwa kuingilia kwake katika shughuli za kanisa hili na yeye ndiye chanzo cha mafarakano ambayo tumekuwa tukiyashuhudia kwa muda," alisema Asiago.Okong'o.
"Anastahili kungatuka mamlakani kwani muda wake wakuhudumu tayari umekamilika." aliongeza Asiago.
Asiago aliongeza kwa kusema kuwa kamwe kanisa hilo halitaruhusu mgawanyiko wa aina yeyote kushuhudiwa kanisani kwa minajili ya mtu aliye na nia yakusambaratisha shughuli za kanisa hilo.
"Kamwe hatutaruhusu kanisa letu kuwa na mgawanyiko wa aina yeyote kwasababu ya mtu aliye na nia mbaya yakusambaratisha uongozi wa kanisa hili na ndio maana yafaa wanaotupinga wawe tayari kukabali maamuzi ya wakristo," aliongezea Asiago.