Shirika la kijamii kwa jina National Citizen Engagement Forum, limetoa wito kwa wakazi wa kaunti ya Nakuru kumakinika mwaka huu wa 2016 na kuhakikisha wanashiriki kikamilifu katika maendeleo ya kaunti.
Mwenyekiti wa NACEF Moses Gitonga alisema kuwa wananchi, kwa mujibu wa katiba, wanajukumu la kuhakikisha viongozi wanawajibika.
"Wakazi wa Nakuru wanatakiwa wajue kwamba katiba inawapa mamlaka,"alisema Gitonga.
Aidha, aliwataka vijana katika kaunti hiyo kuhakikisha wanashiriki katika mambo muhimu yatakayo kuwa ya manufaa kwao.
Gitonga alizungumza wakati wa mahojiano ambapo aliwataka viongozi wa kaunti ya Nakuru kushirikiana ili kuhakikisha maendeleo.