Naibu chansela wa chuo kikuu cha Kisii Professa John Akama ameikosoa vikali tume ya elimu ya vyuo vikuu nchini kwa hatua yake ya kutaka chuo hicho kufunga mabewa yake kumi kwa siku tisini zijazo.
Akihutubu kwenye hafla ya mazishi ya nduguye mbunge wa Borabu Ben Momanyi, Akama alisema kwamba tume ilikiuka mamlaka yake kwa kuchukua hatua hiyo bila ya kushauri usimamizi wa chuo hicho.
“Ni jambo la kuhuzunisha sana kwamba tume ya kuthibiti viwango vya elimu ya vyuo vikuu nchini inaweza kiuka mamlaka yake kwa kuingisha siasa katika elimu kwa kuwa mimi mwenyewe nilipata ufahamu kuhusiana na suala hilo kupitia kwa vyombo vya habari hasa magazeti bila hata ya kutuhuzisha mwanzo," alisema Akama.
Akama aidha aliongeza kwa kusema kuwa huenda hatua hiyo ikasababishwa na uadui mkubwa vyuo vingine nchini vinao kwa chuo hicho kwa sababu chuo
“Kuna mambo fulani yanayojificha kwa kuwa kuna watu mahali fulani wasiofurahia na jinsi chuo ch Kisii kinapoendelea kupanuka, na ni vibaya sana watu kucheza na elimu ya watoto wetuj,” alisema AKama.