Naibu katibu wa chama cha kutetea maslahi ya walimu nchini KNUT James Oteki amejitokeza kuitaka wizara ya elimu nchini kuanzisha upya mpango wa kuorodhesha shule na wanafunzi wanaofanya vyema kwenye mitihani ya kitaifa.
Akizungumza siku ya Jumanne, Oteki alisema kuwa hatua ya kutoorodhesha shule kulingana na matokeo kwenye mitihani ya kitaifa kumepelekea shule nyingi nchini kutofahamu iwapo zemetia fora au la.
"Kama walimu wa Masaba tunaitaka serikali kuanzisha mpango wa kuorodhesha zile shule ambazo hufanya vyema kwenye mitihani ya kitaifa kwa maana hatua hiyo itatusaidia kujipama iwapo tunafanya vyema ikizingatiwa na shule zingine na hata pia kuwapa motisha wanafunzi kutia bidii kwenye masomo," alisema Oteki.
Oteki aidha alimtaka waziri Fred Matiang'i kuanzisha mpango wa kuorodhesha shule kulingana na matokeo kwenye kipindi cha kutangaza matokeo ya kidato cha nne mwaka 2015.
Tungemtaka waziri Matiang'i kuanzisha mpango wa kuorodhesha shule kwenye mitihani ya kitaifa kwa maana yeye pia ni mwalimu anayeelewa umuhimu wa kuorodhesha shule, kwa maana hatua hiyo itawezesha wanafunzi kutia bidii masomoni na hata pia kusaidia shule mbalimbali kujipima," aliongezea Oteki.