Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Licha ya onyo kali kutolewa kwa wahudumu wa magari ya usafiri wa umma kuongeza nauli wakati wa msimu huu wa sikukuu, wasafiri kutoka sehemu mbali mbali wameelezea kutamaushwa kwao na hali ya kuongezwa kwa ada hiyo maradufu.

Uchunguzi uliofanywa na mwandishi huyu, unaonyesha kuwa nauli kutoka Nakuru kulekea Kakamega imefikia shilingi 1,500 ikilinganishwa na hapo awali ambapo ilikuwa shilingi 700. Hata hivyo usafiri kutoka Nakuru kwenda Nairobi haujaadhirika.

Kwingineko, serikali imekashifiwa vikali kwa kuwapa makao wakimbizi wa ndani kwa ndani bandia na kuwaacha taabani walio halali.

Mwenyekiti wa kitaifa wa wakimbizi Peter Kariuki amesema kuwa serikali imepuuza daftari ya walio halali na kutumia iliyowekwa majina ya watu ambao hawakuadhirika na machafuko ya kisiasa.

Akizungumza na mwandishi huyu, Kariuki ameitaka serikali kuelezea mbinu ilizotumia kuwatambua wakimbizi halali, huku akimkashifu kiongozi mmoja kwa kujitangaza kuwa msemaji wa wahanga hao kwa lengo la kujifaidi.