Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Hatua ya mbunge wa Likoni Mwalimu Masoud Mwahima kutangaza kukihama chama cha ODM na kujiunga na chama cha Jubilee inazidi kumtia matatani na sasa Hassan Ndomoko anamtaka ajiuzulu.

Ndomoko ambaye ndiye mwenyekiti wa chama cha ODM tawi dogo la Likoni, Mombasa, amesema Mwahima anafaa kung’atuka ili kutoa nafasi kwa uchaguzi kufanywa kwani tayari amekihama chama kilichompeleka bungeni.

"2002 Mwahima alisimama akabwagwa, 2013 alilia ODM ikampa nafasi akachaguliwa, leo hii anajiona bora kuliko chama kilichomfanya akawa mbunge," alisema Ndomoko.

Ndomoko alisema tayari wamemwandikia barua kinara wa ODM Raila Odinga ili kupata ufafanuzi wa suala hilo kabla kumchukulia hatua Mwahima kwa mujibu wa sheria za chama.

Siku za hivi majuzi Mwahima alitangaza rasmi kukihama chama hicho huku akiwaomba  Wapwani kuufuata mkondo huo akidai Jubilee pekee ndiyo yenye uwezo wa kutatua shida zinazo wakumba.