Ndungu wawili wamefikishwa katika mahakama kuu ya Mombasa kwa kosa la mauaji.
Kati ya Januari 23 na 24, 2016, katika eneo la Mariakani huko Kaloleni, Ramadhani Kaingu Mwaruwa na Swalehe Kaingu Mwaruwa wanadaiwa kumuua Kalama Gona Fondo.
Jaji Martin Muya ameagiza wawili hao kufanyiwa uchunguzi wa umri na akili kabla ya kusomewa mashtaka ya mauaji.
Aidha ameagiza wazuiliwe katika kituo cha polisi cha Mariakani.
Kesi yao itatajwa Februari 11, 2016 baada ya uchunguzi wa akili na umri kukamilika.