Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Mkurugenzi wa mazingira katika kaunti ya Kisii Samson Bokea amewaonya wamiliki wa mikahawa ,baa na makanisa mjini Kisii dhidi ya kufungulia sauti za mziki wa juu mjini humo.

Bokea alisema ni kinyume na sheria miziki kufunguliwa kwa sauti ya juu huku akisema watakaopatikana wakifanya hivyo basi watachukuliwa hatua kali za kisheria.

Akizungumza siku ya Alhamisi mjini Kisii, Bokea alisema serikali ya kaunti ya Kisii hivi maajuzi ilianzisha mahakama itakayowachukulia hatua za kisheria wale wanavunja sheria.