Aliyekuwa mwenyekiti wa LSK kanda ya Bonde la Ufa Bernard Ng'etich ametoa usemi wake kuhusiana na sheria tata ya kumpa rais mamlaka ya kuteua jaji mkuu.
Akizungumza siku ya Alhamisi, Wakili Ng'etich alisema kuwa iwapo sheria hio itakubaliwa, hatua hiyo itakandamiza uhuru wa idara ya mahakama.
"Hii sheria namna ilivyo kwa sasa inaonekana kuipokonya idara ya mahakama uhuru wake kwa kumpa rais mamlaka,” alisema Ng'etich.
Matamshi yake yanajiri siku moja tu baada ya mahakama kuu kudinda kusitisha utekelezaji wa sheria hio inayompa rais mamlaka ya kumteua jaji mkuu.
Siku ya Jumatano, Jaji George Odunga aliamuru pande zote katika kesi hio kuwasilishwa stakabadhi muhimu huku kesi hio ikitarajiwa kuskizwa Januari 13, 2016.