Mbunge wa Bahati Kimani Ngunjiri amesema kuwa watoto wote walio na hamu ya masomo lakini wanatoka familia maskini watafaidika na ufadhili wa masomo.
Akiongea katika shule ya upili ya St Antony Engoshura, Ngunjiri aliahidi kuwa afisi ya CDF itatenga fedha zaidi ili kufadhili masomo kwa watoto wote kutoka familia zisizo na uwezo.
Ngunjiri alikuwa akitoa hundi ya Sh 324, 000 kufaidi wanafunzi 86 kwenye shule hiyo.
“Mimi ni mtu anapenda masomo na ninataka niwahakikishie kuwa tutazidi kufadhili masomo. Hakuna motto kutoka familia maskini atakosa kwenda shule kwa sababu ya karo,” Ngunjiri alisema.
Aidha waalimu wa shule hiyo walisifia mchango wa afisi ya CDF kwenye shule hiyo.
“Mbunge amefanya kazi nzuri, kwa sasa tuko hadi na maji kutokana na mchango wa CDF,” alisema mwalimu mmoja.