Siku chache tu baada ya Waziri wa elimu Fred Matiang'i kuzuru shule kadhaa kaunti ya Nakuru na kuwaonya walimu wazembe, mbunge wa Bahati Kimani Ngunjiri amempongeza waziri huyo.
Akizungumza katika eneo bunge lake, Ngunjiri alisema kuwa ni jambo la busara kwa waziri kuwa makini katika sekta hiyo, huku akiongeza kuwa si walimu wote wazembe, bali baadhi yao wanafaa kuchukuliwa hatua kali.
Kwa mujibu wa Ngunjiri, wizara ya elimu inafaa kuwa macho na baadhi ya walimu wazembe ili kurejesha nidhamu shuleni na kuimarisha matokeo.
"Shule zetu zinaweza tu fanya vyema iwapo walimu watawajibika na tunaona waziri ameanza vyema," alisema Matiang'i.
Itakumbukwa kuwa alipozuru shule kadhaa Njoro na kupata baadhi ya walimu kama hawapo shuleni bila ufahamu walipokuwa, Waziri Matiang'i alisema kuwa sharti wachukuliwe hatua.