Mbunge wa Bahati Kimani Ngunjiri amewataka wakaazi wa eneo bunge la Bahati sawa na kaunti ya Nakuru wajitokeze na kujisajili kama wapiga kura.
Kimani alisema wakaazi hao hawafai kupitwa na huduma hiyo ambayo inaendelea kwa sasa katika maeneo mbalimbali.
Wakenya ambao hawajisajili kupiga kura pamoja na wale wanaotaka kubadili kura zao wanatakiwa kutembelea vituo vya IEBC na kufanya hivyo.
Wanasiasa wamekuwa katika mstari wa mbele kuwataka wananchi wajisajili huku kinyang’anyiro cha mwaka wa 2017 kikikaribia. Shughuli hiyo ya usajili ilianza Jumatatu 15 na inatarajiwa kuendelea kwa mwezi mmoja.