Bodi ya unyunyuziaji maji kitaifa, NIB, imesema kwamba serikali imejikabidhi kusaidia vikundi vya akina mama na vijana katika kujiinua kiuchumi kupitia miradi ya ukulima.
Ijumaa bodi hiyo kwa ushirikiano na mbunge wa Bahati Kimani Ngunjiri, ilipokeza vikundi vya kijamii CBO, vyumba vinane kati ya 12 vya kukuzia mazao (Green House), vikundi ambavyo vimeanzishwa na wakaazi katika katika eneo bunge la Bahati.
Miradi ya vyumba hivyo vya ukulima imekuwa ikifadhiliwa na NIB, kwa ushirikiano wa wizara ya maji na unyunyiziaji.
Mhandisi wa NIB John Kinyanjui, alisema: “Waliofadikika na miradi hii wamepewa usaidizi na ushauri mkubwa kupitia IRRITEC, ambao ni wanakandarasi watalaamu wa kilimo.”
Katika kaunti ya Nakuru, kuna vyumba 37 pekee kama hivyo vya kilimo, vilivyotolewa na NIB idadi ndogo sana ikilinganishwa na Kakamega yenye zaidi ya vyumba 3,000.
Kulingana na mwenyekiti wa kikundi cha ushirika cha Bahati North District, Leah Kamau, kila moja ya mradi huo hutoa nyanya zinazouzwa kwa shilingi elfu 600,000 katika kipindi cha miezi tisa ya mavuno.