Funza ni wadudu wadogo wanaopenda mazingira chafu haswa kwenye vumbi. Wao huishi kwa kufyonza damu. Funza wamekuwa donda sugu kwa familia nyingi katika kaunti ya kisii. 

Share news tips with us here at Hivisasa

Muhudumu wa afya anayepambana na funza kutoka hospitali ya Kisii Level 6, Kepha Nyakundi, alisema kuwa kuna dawa spesheli ya kuwaangamiza funza. 

''Kumwangamiza funza, unahitaji kemikali aina ya Potassium Permanganate, mafuta spesheli ya kuwakamua ngombe aina ya milking salve na suphlon,'' alisema Nyakundi.

Alisema hatua ya kwanza ni kuchanganya potassium na suphlon pamoja na maji kisha unamwosha mwaadhiriwa hadi funza wanaanza kudondoka. Baadaye, unampaka mafuta aina ya milking salve. Mafuta haya husaidia kulainisha ngozi iwe nyorororo kwa funza kudondoka. 

Inasemekana ili hatua hili lifuzu, unahitaji kuirudia kwa wiki moja na funza atakuwa ameangania kabisaa. Baada ya kufanya hivyo, nyunyizia sakafu pamoja na kuta ukitumia dawa ya Actelex ili kuwaangamiza wale ambao huenda wamechificha sakafuni na kuta. Dawa hii ni hatari sana kwa afya ya binadamu kwa hivyo unaponyunyizia hakikisha kwamba chakula kimewekwa mbali ili kuepukana na madhara.

Nyakundi alisema amejitolea kusaidia zile familia ambazo zimeadhirika bila malipo yoyote. Zaidi ya familia 700 katika kaunti ya Kisii zimeadhirika vikali kutokana na wadudu hawa. 

''Kufikia sasa familia 858 zimepokea msaada wa matibabu bila malipo. Vilevile, nimekaza kamba ili kuwaangamiza funza sio kwa kaunti ya kisii tu! Bali Kenya nzima,'' alisema Nyakundi. 

Kulingana na daktari huyu, funza wanaweza kusababisha kifo kwa kufyonza damu na kuuacha mwili kugandana. Amewaomba wakaazi wa kaunti ya Kisii kupiga ripoti katika hospitali ya Kisii Level 6 kwa matibabu ya haraka.