Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Waziri wa usalama wa ndani nchini Joseph Nkaissery ameshtumu vikali mauaji ya wanajeshi wa Kenya KDF waliyoshambuliwa na wanamgambo wa Alshabab katika kambi ya KDF kwenye mpaka wa Kenya na Somalia eneo la El Adde.

Nkaissery amesema kuwa serikali kamwe haitayumbishwa na Alshabab na vita dhidi ya magaidi, wahalifu na wenye itikadi kali vitaendelezwa na akawaonya wanaosambaza picha za mauaji ya wanajeshi hao kuwa watachukulia hatua za kisheria.

Akiongea na wanahabari mjini Mombasa siku ya Jumamosi, Nkaissery amemuagiza Inspekta mkuu generali wa Polisi Joseph Boinnet kuchukua hatua za haraka dhidi ya wanaosambaza picha za maauji ya wanaajeshi wa KDF ili kuimarisha usalama, japo hakugusia idadi ya wanajeshi waliyouwawa.

Wakati uo huo amewaonya wanaoendeleza uuzaji wa pombe haramu na dawa ya kulevya nchini kuwa serikali itakabiliana nao kikamilifu na kusambaratisha biashara hiyo haramu.