Wanafunzi mjini Nakuru wameonywa dhidi ya kuzurura mjini ovyo ovyo haswa wakati wa likizo ya Krismasi.
Kamishna wa kaunti hiyo Joshua Nkanatha amewaonya wanafuzni watakaopatikana wakizurura mjini nyakati za usiku kwamba watakamatwa na kushtakiwa,
Akizungumza afisini mwake jumatatu Nkanatha alisema kuwa hawataruhusu tabia ya vijana kulewa na kupiga kambi katika barabara za mji haswa usiku.
“Kuna tabia ambayo hutokea msimu wa krismasi ambapo vijana hujiingiza katika unywaji wa pombe na kuzurura mjini haswa nyakati za jioni na usiku lakini hilo hatakubali na tunawaonya wale wote wanaofikiria kufanya mambo hayo kuwa chuma chao ki motoni na tutawakamata,” alisema Nkanatha.
Aidha aliwaonya vijana walio chini ya umri wa miaka kumi na minane dhidi ya kuignia katika maeneo ya brurudani yanayouza pombe an kuoneysha sinema za utu uzima.
“Kama wewe ni kijana ambaye hana kitambulisho basi huna sababu ya kuingia katika eneo la burudani kwa sababu ukipatikana huko tutakuweka ndani,” alisema.
Kamishna Nkanatha aliwataka wazazi kutekelea jukumu lao la kuwalea na kuwashauri wanao haswa wakti huu wa likizo ndefu.
“Iwapo wazazi watachukua jukumu lao la kuwashauri watoto wao basi maovu mengi katika jamii tutayamaliza na mimi nawasihi wamenye hivyo wakati huu ambapo watoto wako likizoni,” akasema