Mamlaka ya usafiri na usalama nchini NTSA limeonya dhidi ya kuiingizwa siasa kwa ujenzi wa eneo la kuegesha malori linalonuiwa kujengwa katika eneo la Salgaa jimbo la Nakuru.
Kulingana na mwenyekiti wa mamlaka hayo Lee Kinyanjui ni kuwa eneo hilo linalotarajiwa kujengwa litagharimu mamilioni ya pesa na litakuwa na nafasi ya kuegesha malori mia mbili.
Chini ya mammlaka ya barabara kuu Kenya National Highways Authority (KeNHA) eneo hilo halikujengwa mwaka wa 2015 kutokana na sintofaamu iliyojiri kati ya viongozi na wakaazi wa eneo hilo.
“Eneo hili linakusudiwa kuthibiti malori hususan yale ya matenki ili kupunguza msongamano wa malori hayo na hata kuzuia visa vya dharura vya mioto katika eneo hili,” alisema Kinyanjui.
Huku akizingatia ajali ya mapema mwakani katika eneo hilo Kinyanjui amesema kuwa ujenzi huo vilevile unakusudia kupunguza idadi ya magari mengi sawia na ajali zinatokea katika eneo la Salgaa kutokana na hatari iliyomo katika sehemu ambayo malori mengi huegeshwa kiholela.
Hata hivyo kiongozi huyo amedokeza kuwa mamlaka hayo yanapanga mikakati ya ujenzi wa kiwanda hicho ili kuthibiti hali.
Wakati uo huo Bw Kinyajui ameyataka mamlaka ya kupambana na dawa za kulevya na mivinyo NACADA kuchukulia hatua vituo vinavyouza vileo vinavyoibuka kila kuchao katika eneo hilo.
Hata hivyo kiongozi huyo amewataka madereva kuwa waangalifu na kuzingatia sheria za barabara akisema kutokana na uvunjaji sheria hizo ajali zinazidi kushuhudiwa katika eneo hilo kila kuchao.