Share news tips with us here at Hivisasa

Mamlaka ya usafiri na usalama barabarani NTSA imetakiwa ichunguze leseni za madereva wa magari ya umma.

Mbunge wa Nakuru Magharibi Samuel Arama alisema NTSA inafaa ichukue hatua hiyo kwa madereva wamekosa kutilia maanani kanuni za barabara.

Mbunge huyo alisema sheria ya kasi ya magari pia inafaa kuangaliwa upya.

Wakati huo huo, alitaka mamlaka ya NTSA iangazie chanzo cha ajali nyingi ambazo zinazidi kushuhudiwa humu nchini.