Mwakilishi wa wadi ya Sensi eneo bunge la Kitutu Chache kaunti ya Kisii Onchong’a Nyagaka ameomba wakazi wa wadi hiyo kushirikiana naye kuleta maendeleo zaidi katika wadi hiyo.
Wito huo umetolewa na mwakilishi huyo ambaye alidai kuwa bila ushirikiano kati ya viongozi na wakazi hakuna maendeleo yatafanywa kamwe.
Akizungumza na mwandishi huyu siku ya Alhamisi mjini Kisii Nyagaka alisema kile ambacho wakazi wanahitaji kufanyiwa mbali na maendeleo yale ameratibu kufanya sharti washirikiane naye ili kumwambia huku akiahidi kutimiza ahadi alizotoa katika maendeleo.
Nyagaka alisema atakarabati barabara nyingi za wadi yake huku zile ambazo wakazi wamekuwa wakidai kukarabatiwa kuwa miongoni mwao haswa barabara ya kutoka eneo la Nyakeiri- El Shadai – Engoto –Engoto Goti, Moyare – Nyanchogu na zingine nyingi.
Aidha, Nyagaka alisema miradi ya maji nayo amepanga kuweka na kusema atachimba vizima vya maji katika eneo mabalimbali za wadi hiyo.
“Mimi kama mwakilshi wa wadi nitajaribu kila niwezalo kuhakikisha maendeleo yale niliahidi ya kukarabati barabara kuweka miradi ya maji, kusaidia mayatima na mengine nitayafanya,” alisema Onchong’a Nyagaka mwakilishi wadi.
“Naomba wakazi kushirikiana nami ili hayo yote kuafikiwa kikamilifui na kwa muda unaofaa,” aliongeza Nyagaka.
Wakazi wa wadi hiyo wamekuwa wakimkosoa mwakilishi kwa kutotimiza ahadi alizotoa mapema haswa katika miradi ya maji lakini mwakilishi huyo amesema atafanya.