Share news tips with us here at Hivisasa

Gavana wa Kaunti ya Nyamira John Nyagarama ameahidi kufanya maendeleo zaidi ili kuwanufaisha wakazi wa kaunti hiyo.

Akizungumza siku ya Jumanne katika majengo ya bunge ya kaunti ya Nyamira alipofungua vikao vya bunge hilo baada ya likizo, Nyagarama alisema serikali yake imeweka mikakati kabambe ya kuhakikisha wakazi wa kaunti hiyo wanafanyiwa maendeleo kikamilifu.

Miongoni mwa maendeleo Nyagarama alitangaza kufanya ni ukarabati wa barabara, kuweka miradi ya maji kwa kuchimba visima, kuimarisha sekta ya afya, kukarabatai vyuo vya anuwai miongoni mwa maendeleo mengine.

Nyagarama alisema yeye kama gavana atajaribu kila awezalo kuhakikisha ahadi zote alizotoa atazitimiza kwa wakazi wa kaunti yake.

“Wakati huu serikali yangu itahakikisha kila mradi wa maendeleo umekamilika vizuri katika sehemu mbalimbali za kaunti,” alisema Nyagarama.

Wakati huo huo, Nyagarama aliomba mawaziri wake wote kushirikinana na wawakilishi wadi kuhakikisha miradi yote inafanywa kwa njia ya halali, kuku akikashifu baadhi ya miradi iliyoanzishwa bila kufanya kwa njia ya kiwango kinachostahili.

Nyagarama amekuwa akikosolewa kwa mda mrefu kwa kutofanya maendeleo, huku akitoa ahadi za kutimiza yote aliyoahidi.

“Naomba mawaziri kuhakikisha kila mradi umefanywa kwa njia inayostahili ili pesa za umma kutumika vizuri,” alisisitiza Nyagarama.