Mwenyekiti wa Jomo Kenyatta foundation Walter Nyambati ameiomba serikali ya kitaifa kuwatafutia soko wakulima wa majani chai ili kuwafaidi wakulima hao kupitia mumea huo.
Wito huo umetolewa baada ya kubainika kuwa soko la majani chai lililoko kwa sasa halina faida nyingi kwa wakulima na ata kupelekea wakulima.
Akizungumza siku ya Alhamisi katika eneo la Matunwa wakati ujenzi wa kiwanda kipya cha majani chai kilianzishwa katika eneo hilo la Matunwa, Nyambati aliomba serikali kutafuta soko kwa wakulima wa mmea huo haswa katika nchi za ng’ambo.
“Naomba serikali ya kitaifa ijaribu kila iwezalo kuona kuwa wakulima wetu wa majani chai wanapata faida, kuafikia hilo sharti soko itafutwe ambayo itatoa ufanisi kwa wakulima wetu,” alihoji Nyambati.
Matamshi ya Nyambati yaliungwa mkono na mshauri mkuu wa Benki ya Dunia Charles Mochama ambaye alisema wakati umefika kwa wakulima wa mmea wa majani chai kufaidika.
"Wakulima wetu wamekuwa wakiteseka kwa kukabidhiwa mshahara ambao hautoshi na wakati umefika wakulima wa mmea huo wanastahili kuvuna mapato yaliyo ya juu zaidi,” alisema Mochama.