Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Kijana mwenye umri wa miaka 16 amefikishwa katika mahakama ya watoto jijini Kisumu akikabiliwa na shtaka la kuiba shilingi 150, 000.

Upande wa mashtaka uliifahamisha mahakama kuwa mshtakiwa ambaye jina lake tumelibana kutokana na sheria zinazodhibiti haki za watoto aliiba pesa hizo za mlalamishi ambaye ni nyanya yake kwa jina Siphrosa Ouda Awinda.

Mahakama ilifahamishwa kuwa kijana huyo alitekeleza wizi huo mnamo tarehe Oktoba 7, 2015 katika kijiji cha Kadete eneo la Rabuor jijini Kisumu.

Hakimu mkaazi Angeline Adao wa mahakama ya watoto amesema kesi hiyo itaskizwa tena mnamo tarehe February 23, 2016.