Share news tips with us here at Hivisasa

Chama cha ODM kinatarajiwa kuunda kamati maalumu kuwachunguza wanasiasa waasi wa chama hicho.

Hatua hii ilitangwazwa na Gavana wa Mombasa Hassan Joho alipokuwa akihutubia wananchi wa sehemu hiyo suku ya Jumatano.

Gavana huyo aliwataja wanasiasa hao kama vigeugeu na wasiokuwa na misingi thabiti, na kuongeza kuwa nia yao ni kujikimu kibinafsi wala sio kwa manufaa ya wananchi wao.

Joho amewataka wanasiasa waliokiasi chama hicho kuhama ili uchaguzi mdogo kufanyika kwa haraka kwa mujibu wa katiba.

Hatua hii inajiri baada ya kushudiwa idadi kubwa ya wabunge wa ODM kutangaza wazi kutounga mkono ODM kwenye uchaguzi wa mwaka 2017.