Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Chama cha ODM kimelitaka gazeti moja la humu nchini kuomba msamaha kwa kuripoti kwamba mgombea kiti cha eneo bunge la Malindi kwa tikiti ya ODM William Mtengo anamiliki vyeti gushi.

Chama hicho kilitishia kushtaki usimamizi wa gazeti hilo kwa kile kilichotaja kama kuchapisha propaganda.

Gavana wa Kaunti ya Mombasa Hassan Joho ameitaja ripoti hiyo kama ishara ya wapinzani wao kuogopa kushindwa.

Akizungumza katika wadi ya Shella siku ya Ijumaa, Joho alidai kuwa ripoti hiyo ya vyeti bandia ni mojawapo ya baadhi ya mbinu zinazotumiwa na viongozi wa Jubilee ili kupata ushindi.

Aidha, aliitaja ripoti hiyo kama propaganda na kuitaka tume huru ya uchaguzi nchini IEBC, kuongoza uchaguzi huo kisheria na kuwaonya dhidi ya kupendelea upande wowote.

Hatua hii inajiri baada ya gazeti moja nchini kuandika taarifa kuwa mgombea wa kiti chicho cha ODM, William Mtengo anamiliki vyeti gushi.