Seneta wa kaunti ya Nyamira Kennedy Okong’o ameahidi kuendelea na mradi wake wa kufadhili shule za msingi na za upili kwa kuwapa vitabu pamoja na tarakilishi ili kuinua viwango vya elimu.
Kulingana na Okong’o, ufadhili huo umekuwa kwa miaka minane iliyopita, huku akisema ataendelea hadi aone viwango vya masomo vimeinuka katika.
Akizungumza siku ya Jumanne mjini Nyamira, Okong’o aliomba wanafunzi wote kutia motisha katika mosomo ili kufanya vyema katika mitihani ya kitaifa inapofika.
“Mimi kama seneta wa kaunti hii nitaendelea kufadhili shule za kaunti hii tarakilishi na vitabu ili kuinua viwango vya elimu katika kaunti hii ya Nyamira,” alisema Okong’o.
Aidha, Okongo aliomba wahisani wema kujitokeza kusaidia watoto mayatima na familia maskini ili nao kupata elimu ambayo itawasaidia nyakati zijazo.
“Watoto wetu wanastahili kupata elimu ata wale wa familia maskini na mayatima wanastahili kufadhiliwa kuendela na masomo,” aliongeza okong’o.
Okong’o ameonekana kupigania elimu katika kaunti ya Nyamira katika siku za hivi maajuzi, huku wazazi wa kaunti hiyo wakifurahia yale anayoyafanya.