Mwenyekiti wa ukumbi wa mikutano KICC Omingo Magara amewakosoa wanasiasa wanaolaumu ziara za Rais Uhuru Kenyatta na kusema kuwa ziara hizo zimeleta manufaa katika nchi ya Kenya.
Kulingana na mwenyekiti huyo hakuna haja ya kumlaumu Rais Kenyatta ila kumpongeza kwa juhudi ambazo anaendeleza kufanya kuhakikisha kuwa nchi ya Kenya imepiga hatua katika maendeleo.
Akizungumza siku ya Jumapili katika kanisa la kikatoriki la Tabaka lililoko eneo bunge la Mugirango Kusini kaunti ya Kisii, Magara aliwakosoa vikali wanaolaumu ziara za Kenyatta na kuwaomba kuacha siasa zisizo na maendeleo na kuungana na serikali ili kuleta mandeleo pamoja.
Magara alikosoa muungano wa upinzani CORD kwa siasa mbaya kwa serikali ya Jubilee na kuomba muungano huo unaongozwa na Raila Odinga kukomeza kulaumu serikali kila wakati.
“Ziara za Rais Kenyataa zimeleta manufaa katika nchi ya Kenya, ziara hizo zilimfanya Rais wa umerekani Barrack Obama na papa Francis kufanya ziara nchini na hiyo ndio njia moja ya kuonyesha maendeleo katika taifa letu,” alisema Magara.
“Obama alipotembelea nchi ya Kenya tuliweza kufaidika na pesa ambazo zitaleta maendeleo mengi katika taifa letu na hakuna haja ya kulaumu Rais kwani ziara zake huleta manufaa katika taifa letu kila wakati,” aliongeza Kenyatta.
Matamshi hayo yaliungwa mkono na mwenyekiti wa maktaba nchini Samuel Nyangezo, mwenyekiti wa Jomo Kenyatta foundation Walter Nyambati na mwenyekiti wa kibali Robert Moda ambao walikuwa kwa kanisa hilo na kusema Ziara za Rais ni za maendeleo.
Omingo Magara alikuwa mbunge wa eneo bunge la Mugirango Kusini.