Gavana wa Kaunti ya Kisii James Ongwae amewahimiza wakazi wote wa kaunti hiyo kuhakikisha wamejitokeza kwa wingi wakati wa kupiga kura ili watumie kura zao kuleta uongozi mwema.
Ushauri huo ulitolewa baada ya kubainika kuwa kuna wengi ambao hujisajili na kupata vitambulisho pamoja na kadi za kura, lakini wakati wa kupiga kura unapofika hukaa nyumbani bila kutumia kadi hizo kupiga kura.
Akizungumza siku ya Alhamisi katika mkahawa mmoja mjini Kisii, Ongwae alisema wote ambao watachukua kadi za kura watumie vizuri kupiga kura ili kuleta uongozi wa maendeleo.
“Naomba yeyote anayeshika kura ajaribu ajitokeze wakati wa kura na kupiga kura ili kuchagua viongozi wa kuleta maendeleo,” alisema gavana Ongwae
“Hakuna haja ya mtu kuchukua kura na asitumie kura hiyo kupiga kura, hilo ni jambo na kuhusunisha na kushangaza kupita kiasi,” aliongeza Ongwae.
Wakati huo huo, Ongwae alisema katika kaunti ya Kisii watu walio na vitambulisho wako zaidi ya 800,000, na kuomba kila mmoja kuchukua kitambulisho ili kuwa rahisi ata mtu anapotafuta kitu katika serikali ya kitaifa anapata.
Aidha, Ongwae alisema ni muhimu kwa kila mtu kupiga kura kwa njia ya udemocrasia.