Gavana wa Kaunti ya Kisii James Ongwae amewaomba wazazi wote wa kaunti hiyo kukumbuka masomo wanaposherekea krismasi na mwaka mpya.
Ongwae alisema wazazi wote sharti wakumbuke kuwasomesha watoto wao kwa kuwachukua wanao shuleni baada ya sherehe hizo kwani matokeo ya mitihani ya kitaifa ya darasa la nane na ya kidato cha nne mwaka jana yamekaribia kutangazwa ili watoto kupelekwa shuleni.
Kulingana na Ongwae, elimu ndio msingi wa maisha, na kuna haja ya kila mzazi kumsomesha mtoto wake ikiwa anahitaji maisha yasiyo magumu katika siku sijazo.
Ata hivyo, Ongwae aliomba wakazi wanaposherekea sherehe za msimu huu wakumbuke yajayo kwa kutomaliza pesa haswa za kuwapeleka wanao shuleni mwaka ujao.
Akiongea siku ya Jumatano mjini Kisii, Ongwae aliomba wakazi kuwa na utulivu wakati wa sherehe ili watu kutojeruhiwa kupitia sherehe hizo kwa kuzua vurugu.
“Naomba kila mtu awe mtulivu msimu huu wa sherehe na wazazi mkumbuke kuwachukua watoto wenu shuleni msiwe mnasherekea mkisahau masomo, masomo ndio ngome ya maisha,” alisema Gavana Ongwae.
Aidha, gavana huyo aliomba wale wa kulewa kutolewa zaidi kwani kuna majukumu yanawahitaji katika boma mbalimbali.
Pia aliomba madereva kupunguza mwendo wa kasi barabarani ili kuzuia maafa kupita ajali za barabarani wanapofanya shughuli za uchukuzi.