Gavana wa kaunti ya Kisii James Ongwae ameombwa kutimiza ahadi aliyotoa kwa wakaazi wa eneo bunge la Bomachoge Chache ya kuikarabati babara katika eneo hilo.
Hii ni baada ya Ongwae kuahidi kuwa angeikarabati barabara ya kutoka Kenyenya-Mogonga–Etago, jambo ambalo wakaazi wanadai hajalitimizwa hadi sasa.
Wakizungumza na waandishi wa habari siku ya jumapili katika eneo la Kenyenya, wakaazi hao wakiongozwa na mzee wa kijiji Brian Maiko, walisema gavana aliwahidi kukarabati barabara hiyo lakini kufikia sasa hakuna jambo lolote ambalo limefanywa .
“Gavana Ongwae alipokuja hapa Kenyenya kwa mazishi alisimama mbele ya waombolezaji akakiri kuwa atatukarabati barabara ya Kenyeya–Etago baada ya kuiona ikiwa katika hali mbaya lakini bado hajatimiza ahadi hiyo,” alisema mzee Maiko.
“Tangu siku hiyo tumesubiri laikin hakuna jambo lolote ambalo limefanywa na mvua inaendelea kunyesha hatupiti kwa barabara hii tunamwomaba gavana atuwekee hata mchanga kama amesahau tumemkumbusha ,” aliongezea bwana huyo.
Aidha, wakaazi hao wameiomba serikali ya kaunti ya kutumia pesa zilizotengewa mikasa ambayo itasababishwa na mvua ya El Nino vizuri kwa kukarabati barabara ambazo hazipitiki katika kaunti hiyo.
Alisema hii ni njia moja wapo ya serikali kuonyesha uwasi kwa utumizi wa fedha hizo.
“Kuna pesa zilizotumwa kutoka serikali ya kitaifa pia serikali ya kaunti yetu ikatenga shilingi millioni hamsini ili kukabiliana na mikasa ya mvua ya El Nino, mbona fedha hizo zisitumike kukarabati barabara ambazo ni mbovu? auliza mkaazi Beatrice Omae
“Tunaomba uwazi wa utumizi mema ya pesa hizo uonekane kama viongozi wanajali maslahi ya wapiga kura na wananchi wote kwa ujumla,” alisema Omae.