Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Gavana wa Kaunti ya Kisii James Ongwae amepongeza mahakama kuu nchini kwa kuitikia sekta ya barabara kuwa chini ya uongozi wa kaunti.

Akizungumza siku ya Jumamosi katika sherehe za kuadhimisha siku kuu ya Jamuhuri zilizoandaliwa uwanjani Gusii Stadium, Gavana Ongwae alipongeza mahakama kuu kwa kuokoa wananchi haswa wa sehemu za mashinani ili kupata mahala pa kupita baada ya sekta ya barabara kuitikiwa kuwa chini ya uongozi wa serikali za kaunti.

Ongwae alisema nchi inaelekeakuzuri kufuatia yale ambayo yanaendelea kufanywa kupitia ushirikianao wa serikali ya kitaifa na serikali za ugatuzi.

“Napongeza mahakama kuu kwa kuitikia na kukubalia sekta ya barabara kugatuliwa ili barabara zote ziwe zinakarabatiwa chini ya usimamizi wa serikali za ugatuzi,” alisema Ongwae

“Sasa wanaichi watafaidika pakubwa kwani idadi kubwa ya barabara ambazo ni mbovu ni zile zilikuwa katika serikali ya kitaifa na sasa zitalainishwa na serikali za ugatuzi kwa kukarabatiwa kikamilifu,” aliongeza Ongwae

Wakati huo huo, Ongwae aliomba sekta hiyo kuharakishwa kusimamiwa na serikali za ugatuzi kwani tayari mahakama imepitisha jambo hilo.

“Naomba shughuli za uhamisho wa sekta hiyo kutoka serikali ya kitaifa iweze kuharakishwa na tuanze kufanya kazi inayostahili ili tusaidie wananchi wa kaunti katika sekta ya uchukuzi, na ninapongeza Rais wa kenya Uhuru Kenyatta kwa Juhudi hizo," aliongeza Ongwae.

Ongwae pia aliomba sekta nyingi kuhamishwa kuwa chini ya uongozi wa kaunti, kwani serikali za ugatuzi zimeonekana kuzaa matunda kwa miaka miwili na unusu tangu ziingie mamlakani.