Wito umetolewa kwa wakristo kuendelea kuombea familia ili pawe na umoja na amani.
Akizungumza wakati wa ibada ya Jumapili katika kanisa katoliki la St Peters Mogoon, Padre Jude Kariuki alisema kuwa familia ndio nguzo ya taifa.
"Familia zina umuhimu na sharti ziombewe ili pawe na amani na ustawi mwema," alisema Padre Jude.
Wakati huo huo, alitoa wito kwa wazazi kuwapa mwelekeo mwema watoto wao.
Kwa mujibu wake,vijana wanafaa kukuzwa kwa njia ya mwenyezi Mungu ili wasije wakapotoka.