Share news tips with us here at Hivisasa

Gavana wa Kaunti ya Kisii James Ongwae ameahidi kuongeza hela za basari kutoka million tano hadi million saba katika kila wadi ifikapo mwaka ujao wa 2017.

Kulingana na Ongwae,  atajaribu kila awezalo kuhakikisha watoto wote ambao hawajiwezi kutoka familia maskini na mayatima watafadhiliwa ili kupata elimu.

Aidha, Ongwae alisema kila shule katika Kaunti ya Kisii itafaidika kutokana na pesa hizo ambazo zimetengwa kwa masuala ya ufadhili wa wanafunzi kielimu ili kujiendeleza kimasomo

Akizungumza siku ya Ijumaa mjini Kisii wakati Benki ya Equity tawi la Kisii ilikuwa inawafadhili wanafunzi kujiunga kidato cha kwanza mwaka huu,  Ongwae alisema elimu ndiyo msingi kwa kila mtoto na kuna haja kwa kila mtoto kusoma ili kujisaidia nyakati zijazo.

“Serikali yangu ya kaunti itaendelea kutoa ufadhili kielimu na mwaka huu pesa za basari zilikuwa million tano kwa kila wadi na mwaka ujao nitaongeza hadi million 7 ili idadi kubwa ya watoto kupata fursa ya kusoma,” alisema Ongwae.

Benki ya equity ilifadhili wanafunzi 25 katika kaunti ya Kisii ambao wataendeleza masomo yao baada ya kupata alama zaidi ya 350, huku wa familia maskni na mayatiwa wakipokezwa nafasi ya kwanza.

Aidha Ongwae alipongeza benki hiyo kwa juhudi za kuhakikisha watoto wanapata masomo ili kujisaidia nyakati zijazo.