Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Afisa wa polisi ameiambia mahakama kuwa walipata habari kutoka kwa raia kuwa kulikuwa na wasichana wasita wanaodaiwa kuwa walikuwa na njama ya kujiunga na kundia la al-Shabaab.

Akitoa ushahidi wake siku ya Jumanne, Fundi Njagi, afisa kutoka eneo la Mandera, aliambia mahakama ya Mombasa kuwa baada ya kupata ripoti hiyo, waliwatia mbaroni wasichana watatu pekee, waliokuwa ndani ya basi ikiaminika kuwa walikuwa wanaelekea Somalia katika eneo la El-wak, mpaka wa Kenya na Somalia.

Afisa huyo alisema kuwa wasichana hao watatu walishindwa kuwaeleza maafisa wa usalama kuhusiana na safari yao, hivyo basi wakawakamata na kuwafungulia mashtaka ya kuwa na uhusiano na kundi la al-Shabaab.

Ummulkheir Sadri Abdalla, Khadija Abubakar Abdulkadir na Maryam Said Aboud, walitiwa mbaroni katika eneo la El-waka wakielekea Somalia mnamo Machi 27, 2015, huku Halima Adan akiwakamatwa katika Kaunti ya Machakos.

Kesi hiyo itasikilizwa tena Aprili 29, 2016, mashahidi wengine watatu watakapotoa ushahidi wao.