Share news tips with us here at Hivisasa

Shahidi wa kwanza kwenye kesi ya ugadi na wizi wa mabavu inayowakabili vijana 27 walionaswa katika msikiti wa Musa ameiambia mahakama kuwa walipata bunduki mbili na risasi zaidi ya 25 ndani ya msikiti huo.

Akitoa ushahidi huo katika mahakama ya Mombasa siku ya Jumatano, afisa wa polisi Geoffrey Ouma alisema kuwa walifanikiwa kunasa bunduki mbili, tarakilishi bebe tatu, visu na bendera zenye maandishi ya kiarabu.

Vijana hao 27 walinashwa mwezi Februari 3, 2014 katika msikiti wa Musa baada ya maafisa wa polisi kufanya msako ndani ya msikiti Musa.

Mashahidi wengine watano watatoa ushahidi wao Mei 23, 2016, huku kesi hiyo ikitarajiwa kuendelea wakati huo.