Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Maafisa wa polisi eneo la Diani wanawazuilia raia wawili wa taifa la Bulgeria ambao walikamatwa kwa tuhuma mbalimbali ikiwemo utapeli na ulanguzi wa mihadatari.

Mmoja alikamatwa katika tawi la benki ya Equity eneo la Diani, huku mwenzake aliyetoroka akikamatwa baadaye wakiwa na kadi bandai za benki hiyo.

Afisa mkuu wa polisi eneo la Msambweni Joseph Omija aliyezungumza na wanahabari siku ya Jumamosi alisema kuwa mshukiwa aliyekamtwa katika benki alikuwa akitoa pesa kwa kutumia kadi hiyo bandia.

“Polisi wetu walimkamata mshukiwa katika benki ya Equity tawi la Diani akitoa pesa kwa kutumia kadi bandia hiyo ni wizi na lazima sheria ichukuliwe dhidi yao,” alieleza Omijah.

Maafisa wa polisi wamenasa vipakatilishi vitatu, pistola moja, mashine ya kutengeza kadi za benki na kadi 27 za benki vilipatikana wakijaribu kuendeleza utapeli huo humu nchini sawa na Tanzania.

Washukiwa hao wanatarajiwa kufikishwa mahakamani siku ya Jumatatu kujibu mashtaka dhidi yao.