Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Maafisa wa polisi katika eneo la Likoni, Kaunti ya Mombasa wameanza uchunguzi kubaini mmliki wa gari moja linalodaiwa kuachwa na watu wasiojulikana katika kituo kimoja cha petroli mjini humo siku ya Alhamisi.

Akithibitisha kisa hicho, afisa mkuu wa kitengo cha ujasusi katika eneo hilo, David Siele, alisema kuwa gari hilo aina ya Toyota yenye nambari ya usajali KBN 85BT liliegeshwa katika kituo hicho na watu wasiojulikana na kisha baadaye wakatoroka.

Kulingana na afisa huyo, huenda gari hilo liliibwa au lilitumika kuiba kwingine na kisha kuachwa hapo baada ya kukumbwa na hitilafu za kimtambo.

Siele alisema kuwa walipokezwa taarifa hiyo na wahudumu wa kituo hicho cha petroli amboa waliingiwa na uoga baada ya gari hilo ambalo vioo vyake vimetiwa rangi, kukaa hapo kwa muda mrefu bila mmliki wake kujitokeza.