Polisi katika eneo la Sironga wamemtia mbaroni fundi mmoja wa stima kwa kosa la kupatikana na bidhaa za stima kwenye duka lbaada ya wananchi kuwaarifu maafisa wa polisi. 

Share news tips with us here at Hivisasa

Kulingana na jirani wa mshukiwa huyo, kwa muda mrefu jamaa huyo amekuwa akipeleka bidhaa mbalimbali kwenye duka lake hasaa masaa ya usiku, na wanashuku kwamba huenda bidhaa hizo za stima zikawa za wizi. 

"Jamaa huyo amekuwa akileta bidhaa mbalimbali kwa duka lake hasa masaa ya usiku na tunashuku kwambia huenda bidhaa hizo zikawa za wizi anazozitoa kwenye sehemu zingine na kuzileta kwa duka lake, wakazi hawajui anakotoa friji, pasi za stima, radio na televisheni," alisema jirani huyo.

Akithibitisha kisa hicho, afisa mkuu wa polisi mjini Nyamira Ricoh Ngare alisema kuwa maafisa wa polisi walipokea arifa kutoka kwa wenyeji wa eneo hilo, na walipomhoji mshukiwa ndipo walipobaini kuwa jamaa huyo alikuwa na bidhaa hizo zilizokuwa zimeripotiwa kuibwa kutoka maduka mengine. 

"Tulipata arifa kutoka kwa wananchi, na tulipofuatia tukapata kuwa kwa kweli bidhaa hizo ni baadhi ya zile zilizoripotiwa kuibwa kutoka maduka mengine ya elektroniki," alisema Ngare. 

Afisa huyo aliongeza kusema kuwa tayari wamemtia mbaroni mshukiwa huyo na anazuiliwa kwenye kituo cha polisi cha Nyamira na atafikishwa mahakamani pindi tu uchunguzi utakapo tamatika.

"Tayari tushamtia mbaroni mshukiwa na kwa sasa tumemzuia kwenye kituo cha polisi cha Nyamira akisubiri kufikishwa mahakamani pindi tu uchunguzi utakapotamatika," alisema Ngare.