Share news tips with us here at Hivisasa

Maafisa katika eneo la Weseges kaunti ndogo ya subukia wanamsaka jamaa mmoja anayedaiwa kumdanganya msichana mmoja wa shule moja ya upili ya Tachasis kwa kutumia dawa kabla ya kumnajisi.

Inadaiwa kuwa msichana huyo alikutana na jamaa huyo majira ya asubuhi alipokuwa akielekea shuleni Alhamisi.

Katika mahojiano kwa njia ya simu na mwalimu mkuu Richard Lamulen Akal amesema kuwa pindi mshukiwa alipomsalimia msichana huyo kwa mkono msichana huyo alianza kumfuata kabla ya kupoteza fahamu.

Amesema kuwa msichana huyo alipatikana muda baadaye katika msitu eneo la Solai takriban kilomita 30 kutoka mahala hapo.

"Tuliweza kumtafuta mwanafunzi huyo na tuliweza kumpata kichakani na tukamfikisha katika zahanati ya Wei ambako alikaguliwa," alisema Bw Lomulen.

Amesema kuwa ripoti ya kituo cha matibabu cha Wei zilibaini kuwa msichana huyo alikuwa amenajisiwa.