Maafisa wa polisi mjini Mombasa wamewatia mbaroni washukiwa wawili wanaokisiwa kuhusika na kifo cha afisa mmoja mjini humo siku ya Jumanne.
OCPD wa Likoni Willy Simba amesema washukiwa hao walikamatwa mapema siku ya Jumatano walipojaribu kuvikwepa vizuizi vya maafisa wa polisi.
Simba amesema wawili hao kwa sasa wanahojiwa na maafisa wa upelelezi kabla kuchukuliwa hatua kwa mjibu wa sheria.
Siku ya jumanne, afisa mmoja wa polisi aliripotiwa kuuwawa na watu wasiojulikana katika eneo la Likoni, Mombasa.
Kulingana na DCI wa Likoni David Siele, afisa huyo alikuwa akishindikiza lori ambalo lilikuwa linasafirisha unga mjini humo kabla kuvamiwa na kuhuliwa.
Inadaiwa kuwa washukiwa hao pia walihepa na bundiki aina ya G3 ya afisa huyo pamoja na pesa taslimu shilingi 100,000.