Idara ya polisi mjini Nakuru imekanusha madai ya kuhusika kwa maafisa wake katika kutekwa nyara kwa wafanyibiashara wawili katika eneo la Whitehouse.
Mkuu wa polisi mjini Nakuru Musa Kongoli amesema kuwa hakuna dhibitisho kuwa maafisa wake walihusika na kuwateka nyara watu hao wawili ambao kufikia sasa haijulikani waliko.
Joseph Chege na Simon Wachira walitekwa nyara na watu wliojihami kwenye barabara kuu ya Nakuru-Nyahururu siku ya Ijumaa.
Jamaa za wawili hao pamoja na madereva wa matatu Jumatatu waliandaaa mandamano mjini Nakuru na kuwashtumu polisi kwa kuhisika na utekejai nyara huo.
Lakini Kongoli akiongea Jumanne afisini mwake amekanusha madai hayo na kuwataka wanaoyatoa kutoa ushahidi.
“Kuna watu wanasema kuwa polisi waliwateka nyara wawili hao na ninawataka waje watuelezee vizuri ili tuweze kubaini ukweli. Lakini ninachokijua ni kuwa hakuna polisi aliyehusika na kisa hicho,” Kongoli alisema.
“Tunawatafuta waliotekwa nyara na waliowateka nyara na tunamuomba aliye na ripoti inayoweza kutusaidia aje atusaidie kuwatafuta,” Kongoli alisema.
Haijabainika kilichopelekea kutekwa nyara kwa wawili hao wala waliowateka nyara.
Wawili hao ni wafanyibiashara mjini Nakuru na pia wamewekeza katika sekta ya matatu.