Maafisi wa polisi waliojiami kwa bunduki siku ya Jumatatu, walizivamia kampuni zinazoaminika kumilikiwa na gavana wa kaunti ya Momabsa Ali Hassan Joho na kuwaamuri wafanyikazi kuondoka.
Akizungumza na wanahabari katika eneo la tukio hilo, mkuu wa polisi katika Halmashauri ya Bandari Zacheus Ng’eno alisema maafisa hao walikua wanatekeleza amri ya wakubwa wao.
Aidha, Ng’eno alisema kuwa kampuni hizo za Autoport na Portside hazitaruhusiwa kuendelea na shughuli zake za kawaida hadi uchunguzi utakapo kamilika.
Haya yanajiri wakati tayari wakurugenzi wa kampuni hizo siku ya Jumatatu wiki hii, walipata amri ya mahakama inayoizuia mamlaka ya ukushaji ushuru nchini KRA, dhidi ya kuendelea na uchunguzi dhidi yake.
Kampuni hizo zilifungwa siku ya Alhamisi wiki iliyopita kwa madai ya uingizaji wa bidhaa ghushi nchini pamoja na ukwepaji wa kulipa kodi, madai yaliyopingwa vikali na wasimamizi.